Macron atangaza rasmi kuwania muhula wa pili wa urais.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza rasmi kuwa atawania muhula wa pili katika uchaguzi wa rais wa mwezi Aprili. Kwa muda sasa rais Macron alikuwa ameashiria kuwania kiti hicho katika uchaguzi utakaofanyika kwa awamu mbili ya Aprili 10 na 24 bila ya kutangaza rasmi. Mzozo unaoendelea baina ya Urusi na Ukraine umebadili mipango ya kampeni zake za awali. Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, kiongozi huyo mwenye siasa za wastani ametumia muda mwingi katika mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi wa ulimwengu na washirika wa magharibi. Kura za maoni zinaonyesha kuwa Macron ndiye mgombea anayeongoza katika kinyan'ganyiro hicho. Mgombea wa kihafidhina Valerie Pecresse na wagombea wawili wa mrengo mkali wa kulia, Marine le Pen na Eric Zemmour, wanatarajiwa kuwa wapinzani wake wakuu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii