Tume ya Oktoba 29, kukabidhi ripoti Aprili 23

Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Matukio ya Vurugu kabla na Baada ya Uchaguzi, imesema Alhamisi ya Aprili 23, mwaka huu, itakabidhi ripoti yake kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, baada ya kukamilisha uchunguzi.

Dkt Samia, aliiteuwa tume hiyo Novemba 18, mwaka jana, baada ya kutokea vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali za watu binafsi na miundombinu ya umma siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, mwaka jana.

Hayo yameelezwa leo, Jumanne Aprili 21, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande, alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa katika uchunguzi huo, Jaji Chande amesema tume imewafikia jumla ya watu 63,603, baadhi wakitoa ushahidi, wengine ni wataalamu waliohusika kutoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja mbalimbali.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii