MSHINDI wa Kombe la Dunia mara mbili na Brazil, Cafu amesema anaamini mashindano ya mwaka huu ni wakati muafaka kwa mabingwa hao mara tano kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 24.
Cafu alikuwa nahodha wakati Brazil iliposhinda Kombe la Dunia kwa mara ya tano mwaka 2002, ikiifunga Ujerumani 2-0 katika fainali iliyofanyika huko Yokohama nchni Japan.
Pia alikuwa sehemu ya timu iliyoishinda Italia kwa penalti na kushinda kombe hilo mwaka 1994 huko Pasadena nchini Marekani.
"Pia tumemleta kocha mshindi, Carlo Ancelotti, ambaye ataongeza ukuu wa timu ya taifa ya Brazil."Cafu, ambaye alikuwa beki wa kulia, alisema Brazil tayari ina nguvu katika safu ya kati na ushambuliaji, kwa hiyo Ancelotti amejikita katika kuimarisha ulinzi kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.
Alisema anatumaini mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Junior, mchezaji ambaye mara nyingi hujikuta katika utata, atakuwa bora kwa mashindano hayo.10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime