NCHINI Kenya hivi leo kumekuwepo na maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta ambapo kwa sasa lita ya petroli inauzwa kwa Sh. 197.60 za Kenya (sawa na Sh. 3,953.7) wakati dieseli ikiuzwa kwa Ksh. 196.63 (sawa na Sh. 3,934.29) na mafuta taa yakiuzwa kwa Ksh. 152.78 (sawa na Sh. 3,056.91).
Maandamano hayo yanatarajiwa kuongozwa na vijana wa Gen Z, wanaharakati pamoja na Wakenya wengine wanaoituhumu serikali kushindwa kuwakinga dhidi ya makali yanayotokana na kupanda kwa bei ya mafuta.
Tangu kutangazwa kwa bei mpya wiki iliopita na licha ya juhudi za serikali kuondoa ushuru wa thamani kwenye mafuta kwa Sh. tisa, baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakitoa wito kwa wenzao kujitokeza kulalamikia ongezeko hilo.
Ingawa wanaopanga kuandamana wanasema kupanda kwa bei ya mafuta kumewaongezea mzigo wa gharama za maisha ikumbukwe kuwa mwaka wa 2024, vijana wa Gen Z walishirki maandamano makubwa ya kupinga muswada tata wa fedha, maandamano ambayo kwa sehemu kubwa yalipangwa kupitia mitandao ya kijamii.
Hata hivyo ilielezwa kuwa leo Jeshi la Polisi lilionya kuwachukulia hatua waandamanaji ambao hawajatoa taarifa, onyo linaloibua wasiwasi wa kutokea vurugu ikiwa raia watajitokeza.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime