Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya kujadili mizozo

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya watakutana Jumanne kujadili kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati pamoja na uungwaji mkono kwa Ukraine inayoendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

 Mawaziri hao watampokea kwa mazungumzo huko Luxembourg Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam atakayeelezea hali ilivyo nchini mwake kufuatia mzozo na Israel, huku wakizungumza pia kwa njia ya video na mwenzao wa Ukraine Andrii Sybiha.

Hata hivyo wanadiplomasia hao wakuu wa Ulaya wanatarajiwa pia kujadiliana kuhusu vita vya Iran na athari zake pana za kikanda, ikiwa ni pamoja na  mvutano unaoendelea katika Mlango-Bahari wa Hormuz .

Aidha katika ajenda pia kuna mchango wa EU katika mchakato wa amani kati ya Armenia na Azerbaijan pamoja na hali ilivyo nchini Georgia.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii