Mkuu wa IAEA Grossi kwenda Iran Jumamosi

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki - IAEA, Rafael Grossi, atakwenda Iran siku ya Jumamosi kufanya mikutano na maafisa waandamizi wa Iran. Msemaji wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu yake mjini Vienna, amesema Grossi kisha atakuwa na kikao cha waandishi wa habari baada ya kurejea Austria. Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Grossi kuapa kuwa IAEA haitawahi kuwachana na jitihada zake za kuitaka Iran kufafanua uwepo wa awali wa nyenzo za nyuklia katika maeneo kadhaa ambayo hayajatangazwa. Iran imesema kufungwa kwa uchunguzi huo ni muhimu ili kufikia makubaliano ya kuufufua mwafaka wa 2015 na madola yenye nguvu duniani kuhusu mpango wake wa nyuklia. Mazungumzo kuhusu mkataba huo mjini Vienna yanaonekana kuwa katika hatua muhimu, huku siku kadhaa zijazo zikitarajiwa kuamua kama yatafanikiwa au yatashindwa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii