DRC na Uganda zawaokoa mateka 200 waliokuwa mikononi mwa ADF

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakishirikiana na wale wa Uganda walifanikiwa wiki iliyopita kuwaokoa raia wasiopungua 200 wakati wa operesheni kwenye kambi ya wanamgambo wa itikadi kali mashariki mwa DRC.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu na Msemaji wa Jeshi la Uganda Chris Magezi aliyetaja kuwa watu hao walikuwa wameshikiliwa mateka katika kambi iliyo kando ya Mto Epulu na waasi wa ADF wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS na wengi wao walikuwa wagonjwa.

Hata hivyo kulingana na Umoja wa Mataifa, ADF imewaua maelfu ya raia mashariki mwa Kongo tangu mwaka 2014 huku ikihusika pia na utekaji nyara wa idadi kubwa ya raia na kuwalazimisha mateka wa kike kuolewa na wapiganaji.

Aidha mnamo mwaka 2021, Uganda iliwatuma wanajeshi wake nchini Kongo kuisaidia serikali ya Kinshasa kupambana na kundi hilo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii