Wanajeshi wa Urusi waingia katika bandari muhimu ya Kherson, Ukraine

Wanajeshi wa Urusi wameingia leo katikati ya mji wa bandari wa Kherson nchini Ukraine, siku moja baada ya madai yanayokinzana kuhusu kama Moscow imeukamata mji wowote mkubwa nchini humo kwa mara ya kwanza katika uvamizi wake wa siku nane. Meya wa mji huo Igor Kolykhayev amesema jana usiku kuwa askari wa Urusi wako mitaani na wameingia katika jengo la baraza la jiji. Ametoa wito kwa raia kutembea mitaani saa mchana pekee na katika vikundi vidogovidogo. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema iliukamata mji wa Kherson jana lakini mshauri wa Rais wa Ukraine alijibu kuwa wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kuilinda bandari hiyo ya Bahari Nyeusi yenye karibu watu 250,000. Wanajeshi wa Urusi bado hawajaiangusha serikali mjini Kyiv lakini maelfu ya watu wanaripotiwa kuuawa au kujeruhiwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii