Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa Kumi na Nne, anatarajiwa kuwasili nchini Cameroon leo, akitokea nchini Algeria anakotamatisha ziara yake siku ya Jumatano.
Papa Leo atakutana na rais Paul Biya, katika ziara yake ya siku nne kwenye nchi hiyo ya Afrika ya Kati, ambayo idadi kubwa ya raia wake wanazungumza Kifaransa.
Aidha, atazuru Bamenda, katika jimbo la Ambazonia, ambalo wenyeji wake wanazungumza Kiingereza na limekuwa kwenye vita kwa miaka mingi na jeshi la Cameroon, likitaka kujitenga na kujitawala.
Vita katika jimbo hilo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 kufikia mwaka 2024 kwa mujibu wa mashirika yasiyokuwa ya
Akiwa Bamenda, Papa Leo anatarajiwa kuhimiza amani, katika nchi hiyo ambayo inaendelea kushuhudia utawala wa muda mrefu wa rais Biya mwenye umri wa miaka 93.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani, alianzia ziara yake nchini Algeria siku ya Jumatatu, na kabla ya kuelekea Angola siku ya Jumamosi, anatarajiwa kuongoza misa ya maelfu ya watu jijini Douala nchini Cameroon siku ya Ijumaa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime