Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar, amethibitisha leo kuwa nchi yake inasimamia mawasiliano kati ya Marekani na Iran ili kupunguza mvutano na kutafuta kumaliza vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.
Kwenye chapisho katika mtandao wa X, Dar amesema kumekuwa na uvumi wa vyombo vya habari kuhusu mazungumzo ya amani ya kumaliza mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa kiukweli, mazungumzo yasio ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yanafanyika kupitia usimamizi wa Pakistan.
Katika hatua nyingine, mawaziri wa kundi la Hezbollah na mshirika wake Amal wamesusia leo kikao cha baraza la mawaziri la Lebanon, wakilalamikia hatua ya serikali ya kutangaza kuwa balozi wa Iran ni mtu asiyefaa kuwa nchini humo. Haya ni kwa mujibu wa afisa wa Lebanon
Hatua hizi za sasa zinakuja wakati Rais Trump akiendelea kutumia mtandao wake wa Truth Social kutangaza vitisho dhidi ya Iran anayoitaka kukubaliana haraka na matakwa yake.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime