Watu 20 wafariki Tanzania kufuatia maporomoko ya ardhi

Watu wasiopungua 20 wamefariki kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Mbeya, kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa ilioambatana na upepo mkali.

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu ambako maafa hayo yalitokea siku ya Jumatano, amesema  maporomoko hayo yalisababisha pia uharibu  wa nyumba kadhaa, huku idadi ya vifo ikihofiwa kuongezeka.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania imetabiri mvua kubwa katika sehemu nyingi za nchi hiyo hadi Jumanne ijayo. Eneo la Afrika Mashariki limekumbwa kwa wiki kadhaa sasa na mvua kubwa ambazo mwezi huu zimesababisha vifo vya watu 81 na kuwahamisha maelfu ya wengine katika nchi jirani ya Kenya.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii