Wizara
ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya
makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na
kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.
Utiaji
saini huo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri
Mahimbali na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara –
Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem.
Mradi uliolengwa katika Hati ya
Makubaliano husika ni kuendeleza miundombinu ya kitaifa iliyo bora na
ya kisasa ya kupokea na kuhifadhi mafuta na gesi ambayo itatumika katika
kuboresha sekta ya mafuta na gesi nchini na katika ukanda mzima wa
Afrika Mashariki.
Tukio hili lilifanyika tarehe 27 Februari,
2022 katika Kikao cha Kibiashara kilichofanyika huko Dubai – Umoja wa
Falme za Kiarabu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem (kushoto) wakiwa katika zoezi la kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.