Rais Biya amteua mtoto wake kuwa Makamu wa Rais

Rais wa Cameroon, Paul Biya, amemteua mwanawe Franck Emmanuel Biya kuwa Makamu wa Rais, kufuatia kuanzishwa kwa nafasi hiyo mpya ambayo haikuwepo nchini humo tangu mwaka 1972.

Uteuzi huo umefanyika sambamba na mabadiliko ya kikatiba yaliyoipa nafasi ya Makamu wa Rais mamlaka makubwa, ikiwa ni pamoja na kurithi urais moja kwa moja endapo rais aliyepo madarakani atafariki dunia, kujiuzulu au kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa, hatua hiyo inaonekana kama mkakati wa kumwandaa Franck Biya kurithi madaraka, hasa ikizingatiwa kuwa Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 93 amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani aliye madarakani kwa sasa.

Aidha, Franck Biya ameripotiwa kupewa majukumu muhimu ndani ya mfumo wa ulinzi wa nchi, hatua inayoongeza ushawishi wake katika masuala ya kisiasa na kijeshi nchini humo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii