Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari
ya siku tatu kuhusu uwezekano wa mvua kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko
katika baadhi ya mikoa ya ukanda wa Pwani, ikiwemo Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 7, 2026, mvua hizo
zinatarajiwa kuanza kesho Jumatano hadi Ijumaa, zikihusisha mikoa ya Lindi,
Mtwara, Tanga na Pwani pamoja na Jiji la Dar es Salaam, sambamba na visiwa vya
Unguja na Pemba.
AidhaTMA
imeeleza kuwa uwezekano wa mvua hizo pamoja na athari zake uko katika kiwango
cha kati, huku wananchi wakitakiwa kuchukua tahadhari zote muhimu ili kuepuka
madhara yanayoweza kujitokeza.
“Kuanzia
kesho hadi Ijumaa, mvua zinatarajiwa kunyesha katika maeneo tajwa. Uwezekano na
athari zake zipo katika kiwango cha kati,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo, mamlaka hiyo imeonya kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi, hivyo wananchi wanashauriwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kuchukua hatua za kujikinga.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime