MLvutano umeibuka nchini DRC, baada ya kambi ya rais ikitaka kiongozi wao, ambaye ni rais wa Jamhuri kuwania muhula wa tatu wakati wa sherehe za kuwapokea wachezaji wa timu ya taifa ya soka ilipokuwa ikirudi nyumbani baada ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026. Upinzani unaonyesha kwamba ushindi wa timu ya taifa hauendani na maslahi binafsi ya mtu mmoja.
"Moja kwa moja hadi 3": Kauli mbiu hii kutoka kwa chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inayomtaka rais Félix Tshisekedi kugombea muhula wa tatu, imeibuka tena wasiwasi siku ya Jumapili wakati wa kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa ya soka, Leopards, baada ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026.
Ujumbe huu wa kisiasa umezua utata katikati ya sherehe za michezo katika nchi ambapo upinzani unashutumu hili kama jaribio la kutumia vibaya hali hiyo.
Prince Epenge, msemaji wa muungano wa Lamuka, ana wasiwasi na anabaini kwamba chama cha rais kinaichukulia Leopards kama nguzo muhimu kwake: "Jukumu liko kwa UDPS, ambayo inawagawanya raia wa Kongo, kupitia ushindi wa timu ya taifa ya soka, Leopards, na kujaribu kubinafsisha timu hii ya kitaifa ambayo ni ya Wakongo wote."
Kwa upande wake, Olivier Kamitatu, msemaji wa kiongozi wa upinzani Moïse Katumbi, amelaani mkakati wa kambi ya rais: "Hili si tu ni tusi kwa mpira wa miguu, bali pia ni usaliti kwa raia wa Kongo. Wakongo wanahitaji ushindi, hakika, lakini zaidi ya yote wanahitaji amani, utulivu, barabara, maji, umeme, mishahara mizuri kwa kila mtu, na kazi.
Kuamini kwamba mechi ya mpira wa miguu inaweza kubadilisha taifa ni kuonyesha kutokomaa kisiasa na hili ni kosa kubwa. Kwa uwazi na tuseme tu, Ensemble pour la République inasema hapana kwa udanganyifu huu. Mtu hawezi kuchanganya maslahi yako binafsi na maslahi ya taifa zima."
Deo Bizibu Balola, naibu katibu mkuu wa chama cha rais, amejibu: "Hapa ndipo upinzani unapaswa kuelewa kwamba, ili kutoa sifa pale inapostahili, ushindi huu ulipatikana chini ya utawala wa Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, chini ya uongozi wake. Bonasi za wachezaji zinalipwa, wachezaji hawalalamiki tena, na makocha wanalipwa. Waliwekwa kwenye mazingira yaliyowezesha timu ya taifa ya soka kupata ushindi."
Ingawa siku ya Jumapi akitolewa wito wa kuwania muhula wa tatu wakati wa mkutano katika jengo la Bunge, rais alipuuzia suala hilo, akisema kwamba siku hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya mapokezi kwa Leopards baada ya kufanya vizuri.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime