Bei ya mafuta yazidi kupaa duniani kutokana na vita vya Iran

Pipa moja la mafuta ghafi limeuzwa dola 110.34 hadi 113.67 kutegemea na eneo ambalo ununuzi huo umefanyika. Bei hiyo ni ongezeko la asilimia 0.5 hadi 1.1 kutoka kwenye bei ya masaa 24 yaliyopita.

Bei ya mafuta imeendelea kupaa hivi leo siku ya Jumanne wakati Rais wa Marekani Donald Trump akiendelea kutoa vitisho kwa Iran na kuapa kuchukua hatua kali ikiwa nchi hiyo itashindwa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, eneo ambalo ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Pipa moja la mafuta ghafi limeuzwa dola 110.34 hadi 113.67 kutegemea na eneo ambalo ununuzi huo umefanyika. Bei hiyo ni ongezeko la asilimia 0.5 hadi 1.1 kutoka kwenye bei ya masaa 24 yaliyopita.

Aidha vikosi vya Iran viliufunga Mlango-Bahari wa Hormuz baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi dhidi yao mnamo Februari 28, na kuvuruga utaratibu mzima wa usafirishaji wa nishati hiyo.

Hata hivyo wakati bei hiyo ya mafuta ikiendelea kupaa hali bado ni ya wasiwasi na pande zote zimeendelea kushambuliana.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii