Iran yaripoti kuangusha ndege za kivita za Marekani aina ya C- 130

Iran imesema imeangusha ndege mbili za kivita za Marekani, aina ya C-130 na helikopta mbili katika angaa lake, wakati huu vita vikiendelea.

Madai haya ya Iran yanakuja, baada ya rais Donald Trump kusema mwanajeshi wa Marekani aliyetoweka, baada ya kuanguishwa kwa ndege ya kivita, ameokolewa na yupo salama.

Hata hivyo, Trump kupitia mitandao yake ya kijamii, ameongeza kuwa, mwanajeshi huyo wa Marekani, amejeruhiwa vibaya, baada ya ndege ya kivita aina ya F-15 kuagushwa kwenye milima ya Iran.

Katika hatua nyingine, Trump ameonya kuwa miundo mbinu ya nishati na madaraja ya Iran yatashambuliwa na kuharibiwa iwapo eneo la mlango wa Bahari ya Hormuz, haitafunguliwa kufikia siku ya Jumatatu.

Licha ya tishio hili la Trump, Iran inaonekana kutotishika na haioneshi dalili za kurudi nyuma, ikiendelea kushambulia miundo mbinu za kiuchumi katika mataifa ya Ghuba, yaliyo na wanajeshi wa Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii