Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF), amezua mjadala mkubwa kimataifa baada ya kutoa kauli kali dhidi ya Iran kupitia ukurasa wake wa X mnamo Aprili 2, 2026.
Katika ujumbe huo, Muhoozi aliitaka Iran iombe radhi kwa Uganda ndani ya muda wa siku saba, hatua iliyosababisha taharuki na maswali makubwa kuhusu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Aidha, Jenerali huyo aliashiria kuwa hakuna taifa lolote duniani lenye uwezo wa kushinda kijeshi UPDF.
Mbali na onyo hilo, Jenerali Muhoozi alifichua kuwa vyombo vya usalama vya Uganda vimeshika watu aliowataja kama wapelelezi wa Iran waliokuwa wakifanya shughuli ndani ya nchi hiyo.
Hata hivyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu hali ya kukamatwa kwao au ushahidi unaounga mkono madai hayo.
Kauli za Muhoozi zimeibua mjadala mkali kimataifa huku wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wakionya kwamba hatua zinazochukua miongoni mwa viongozi wa kijeshi zinaweza kuongeza mvutano katika eneo zima la Mashariki ya Kati.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime