Iran:Tutapambana hadi maadui wasalimu amri

Iran imesisitiza kuwa itaendelea na vita hadi maadui wake watakaposalimu amri, huku ikikanusha vikali madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba uwezo wake wa kijeshi umedhoofishwa kwa kiwango kikubwa.

Katika taarifa ya hivi karibuni, jeshi la Iran limeonya kuwa maadui wake wanapaswa kutarajia hatua kali zaidi, likionyesha kuwa bado lina uwezo wa kujibu mashambulizi na kulinda maslahi yake ya kitaifa.

Kauli hiyo inakuja wakati mvutano ukiendelea kuongezeka kati ya mataifa hayo mawili, huku mashambulizi na vitisho vikiongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati, hali inayozua hofu ya kupanuka kwa vita. 

Kwa upande wake, Trump amesema Marekani iko karibu kufikia malengo yake yote ya kijeshi, akidai kuwa operesheni hiyo inaweza kukamilika ndani ya muda mfupi huku akisisitiza nguvu ya kijeshi ya nchi yake. 

Hata hivyo, kauli kinzani kutoka pande zote zinaonyesha hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wa vita hivyo, huku wachambuzi wakieleza kuwa mgogoro huo unaweza kuendelea au hata kuongezeka zaidi iwapo suluhu ya kidiplomasia haitapatikana haraka.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii