Watoto wanne wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa visu katika shule moja ya chekechea jijini Kampala.
Kwa mujibu wa Polisi nchini Uganda, mshambuliaji huyo ambaye ni mwanaume aliingia shuleni kwa kujifanya mzazi, kabla ya kutekeleza shambulio hilo dhidi ya watoto waliokuwa na umri wa kati ya miaka miwili hadi mitatu.
Hata hivyo tukio hilo limetajwa kushtua jamii na kuzua hofu kubwa kuhusu usalama wa watoto katika taasisi za elimu ya awali, huku mamlaka zikiahidi kuchunguza kwa kina na kuimarisha ulinzi katika shule zote.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime