Benki Kuu ya Tanzania Yasitisha Uuzaji wa Dhahabu

Benki Kuu ya Tanzania imesitisha kwa muda mpango wa kuuza sehemu ya akiba yake ya dhahabu kufuatia kushuka kwa bei katika soko la dunia.

Akizungumza, Gavana Emmanuel Tutuba alisema benki hiyo imeamua kusubiri hadi bei zitakapotengamaa, licha ya awali kupanga kuuza dhahabu hiyo ilipokaribia dola 5,500 kwa wakia.

Hatua hiyo inaonyesha tahadhari ya benki hiyo katika kulinda thamani ya akiba yake wakati wa mabadiliko ya soko la kimataifa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii