Goncalo Inacio Amekubali Kusaini Mkataba Mpya

Mlinzi wa Sporting Lisbon mreno Goncalo Inacio amekubali kusaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akiwaniwa na Newcastle United katika dirisha la mwezi Januari. (Fabrizio Romano)

Klabu za Real Sociedad na Atalanta zinamuwania kwa mkopo mlinzi wa kushoto mgiriki Dimitris Giannoulis kutoka Norwich City. (Norfolk Live)

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ameiambia klabu hiyo kumpa mikoba ya ukocha, kocha wa sasa wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone. (Goal)

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii