Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie kwa uhamisho huru wakati mkataba wa nyota huyo wa AC Milan mwenye umri wa miaka 25 utakapomalizika. (Sport - in Spanish)
Newcastle United ilishindwa kumsajili mlinzi wa Uholanzi, Sven Botman mwezi Januari, na kinda huyo mwenye miaka 22 ambaye anahusishwa pia na Tottenham, anatarajia kujiunga na AC Milan katika majira yajayo ya joto. (Todofichajes)
Andreas
Christensen ameelezea suala lake ndani ya Chelsea ni "gumu", huku
mkataba wa mlinzi huyo wa Denmark mwenye miaka 25 ukielekea ukingoni
mwisho mwa msimu. (90 Min)