Marekani yaidhinisha mauzo ya muda ya mafuta ya Urusi

Serikali ya Marekani imelegeza kwa muda vikwazo vyake vya kiuchumi dhidi ya Urusi kwa kuruhusu mafuta yake yaliyotelekezwa kwa sasa baharini kuuziwa India.

Aidha idara ya Udhibiti wa Mali za Kigeni kwenye Wizara ya Fedha ya Marekani ilitowa hapo jana kibali kinachoruhusu kuuzwa na kufikishwa mafuta ghafi na bidhaa za petroli za Urusi hadi Aprili 3 mwaka huu.

Waziri wa Fedha Scott Bessent amesema ruhusa hiyo itawezesha mafuta kuendelea kuingia kwenye soko la dunia na kuiondolea India mbinyo wa nishati kufuatia kile alichokiita "jaribio la Iran kuuteka nyara mfumo wa nishati duniani."

Hata hivyo awali, India ilikuwa imesema ingeacha kununua mafuta ya Urusi kama sehemu ya makubaliano yake ya kibiashara na Marekani Mnamo mwezi Novemba, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza vikwazo  dhidi ya kampuni kubwa za mafuta za Urusi, akidai ni njia ya kuilazimisha Moscow kukomesha vita vyake dhidi ya Ukraine.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii