Mke wa rais wa Iraq akataa Wakurdi kuingizwa vitani Iran

Katika tukio la nadra, mke wa Rais Abdul Latif Rashid wa Iran amejitokeza hadharani kupinga uwezekano wowote wa wapiganaji wa Kikurdi kuishambulia Iran.

Shanaz Ibrahim Ahmed, ambaye mwenyewe ni Mkurdi, ameandika kupitia mtandao wa X kwamba Wakurdi waachwe kuhusishwa na vita visivyokuwa vyao, akisema wao "si bunduki za kukodishwa."

Mke huyo wa rais wa Iraq amesema Wakurdi huwa wanakumbukwa pale tu nguvu na muhanga wao unapohitajika, lakini haiwezekani tena kutumika kama chambo cha mataifa yenye nguvu duniani.

Kauli ya Shanaz Ibrahim inakuja huku kukiwa na ripoti kwamba Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiwashawishi Wakurdi kuingia vita vya ardhini dhidi ya Iran.

Trump anaripotiwa kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi kadhaa wa Kikurdi akiwaahidi uungaji mkono kwa upande wake Shanaz alikumbusha kuwa kwenye vita vya Ghuba vya mwaka 1990 hadi 1991, rais wa wakati huo wa Marekani, George Bush, aliwataka Wakurdi wapambane na Rais Saddam Hussein wa Iraq, lakini kisha walitelekezwa na matokeo yake makumi kwa maelfu waliuawa.

Aidha hali  hiyo imetokea kwa Wakurdi wa Syria waliokuwa bega kwa bega na Marekani dhidi ya kundi lijiitalo Dola la Kiislamu, lakini mara baada ya utawala wa Bashar Assad kuanguka, nao wametupwa mkono.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii