Vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran vikiingia siku yake ya saba leo, Israel ikisema imeanzisha awamu mpya ya mashambulizi mapana zaidi dhidi ya miundombinu ya utawala mjini Tehran alfajiri ya leo.
Picha zilizorushwa na shirika la habari la AFP zinaonesha majengo na magari yaliyotekezwa kwa moto mjini Tehran, huku moshi ukifuka kwenye baadhi yake.
Hayo yakijiri, Azerbaijan imeonya kwamba mashambulizi ya droni dhidi ya uwanja wake wa ndege hapo jana hayatapita bila kujibiwa, ikiongeza wasiwasi wa nchi nyengine kujiunga na vita hivyo.
Tehran imekanusha vikali kuhusika na mashambulizi dhidi ya jirani yake huyo na badala yake imeituhumu Israel, lakini hilo halikumzuwia Rais Ilham Aliyev, mshirika mkubwa wa Israel, kuishutumu Iran kwa kile alichokiita "ugaidi."
Hata hivyo shirika la utangazaji la Iran limesema idadi ya watu waliouawa kutokana na mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyoanza Jumamosi, sasa imefikia 1,230 ingawa Marekani, kwa upande wake, imeripoti mwanajeshi wake wa sita kuuawa tangu ilipoanza uchokozi wake.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime