Mwalimu Amuoa Mwanafunzi wake wa Zamani Katika Karamu ya Kufana.

Aliyekuwa kiranja mkuu wa Orient Academy Group of School, Boji-Boji, Stephanie Ebere Odili amefunga pingu za maisha na mwalimu wake wa zamani wa shule ya upili, Sammy Anslem Chuks.
Mapenzi Kipofu: Mwalimu Amuoa Mwanafunzi wake wa Zamani Katika Karamu ya Kufana
Ripoti ya Ika Weekly Newspaper iliripoti Jumapili, Februari 27, kuwa Sammy alikutana na Stephanie mwaka wa 2013, alipokuwa akifanya mazoezi ya kuwa mwalimu.
Akielezea ndoa yake na Stephanie, Sammy ambaye ni mfanyabiashara alisema ni ndoto iliyotimia, akifafanua kwamba kile kilichoanza kama mzaha wa watoto sasa ni ukweli.
Sammy alitoa shukrani za dhati kwa mfumo wa elimu wa Nigeria kwa kumleta pamoja na ubavu wake.
Sammy pia aliwashauri vijana wenye taswira kuwa elimu ni ulaghai kwamba ilimpa zawadi bora zaidi maishani.
"Mke wangu amebaki kuwa mafanikio bora niliyoyapata wakati wa mazoezi yangu ya ualimu, licha ya kwamba walimu wa TP hawalipwi malipo ya utumishi wao. Niliondoka Orient Academy Group of School nikitafuta ubavu wangu... "
"Kwa yote mke wangu ni baraka kubwa sana kwangu.Na namshukuru Mungu kwa kunijalia neema ya kumsubiri amalize elimu yake ya sekondari na ya juu. Kikamilifu upendo tunaoshiriki umetuweka pamoja kwamba licha ya kusubiri kwa muda mrefu, hatujakata tamaa,” alisema
Akizungumzia ndoa yao, Stephanie aliwashauri makapera kutokuwa viruka njia wanapotafuta uvavu wao na kuwa na udhibiti badala ya kuruka kutoka kwa mwanamume mmoja hadi kwa mwingine.
Alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kutimiza ndoto yao ya kuwa mke na mume.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii