Aliyekuwa mwanamfalme Andrew aachiwa uchunguzi ukiendelea

Mwanamfalme huyo wa zamani Alhamis alikamatwa na kuzuiliwa kwa masaa kadhaa kwa ukosefu wa nidhamu na madai ya uhusiano wake na raia wa Marekani Jeffrey Epstein aliyekuwa anakabiliwa na madai ya dhulma za kingono kabla kujitoa uhai.

Mara baada ya kukamatwa kwa Andrew,kakake Mfalme Charles III alitoa taarifa fupi iliyosema, "ni lazima sheria ifuate mkondo wake."

Kukamatwa kwa Andrew ni pigo jengine kwake baada ya kuvuliwa hadhi yake ya uanamfalme mwaka 2025 na kutimuliwa kutoka kwenye makaazi ya kifalme ya Windsor aliyokuwa ameishi kwa zaidi ya miongo miwili.

Hii ndiyo mara ya kwanza katika historia ya familia ya Kifalme ya Uingereza kwa mwanamfalme kukamatwa.

Andrew awali alikanusha kufanya makosa yoyote katika mahusiano yake na Epstein.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii