Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaarifu wateja wake pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mwanza kuwa kutakuwa na zoezi la maboresho ya miundombinu ya umeme katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo kuanzia kesho.
Maboresho hayo yanalenga kuongeza ufanisi wa huduma ya umeme, kupunguza hitilafu za mara kwa mara na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na taasisi za kijamii na kiuchumi.
Kpatika kipindi cha utekelezaji wa kazi hizo, baadhi ya maeneo yanaweza kukumbwa na kukatika kwa umeme kwa muda, hali ambayo TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Aidha TANESCO imewataka wateja kuchukua tahadhari zinazostahili wakati wa zoezi hilo, ikiwemo kuzima vifaa vya umeme ili kuepuka uharibifu pindi huduma itakaporejea.
Hata hivyo shirika hilo limesema maboresho hayo ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma kwa wateja na kuunga mkono maendeleo ya mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime