Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu, amesema mipango ya maendeleo katika sekta ya utalii haipaswi kuchanganywa na hoja za kidini, akisisitiza kuwa miradi ya kimkakati inapaswa kutekelezwa kwa masilahi mapana ya Taifa.
Spika Zungu ametoa kauli hiyo leo Februari 6 mwaka huu akieleza kuwa maendeleo yanahitaji mtazamo wa kitaifa badala ya misimamo ya kidini, kwa kuwa “hakuna udini kwenye fedha wala kwenye maendeleo.”
Akitolea mfano wa historia ya Papa Leo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, aliyewahi kuhudumu katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ikiwamo Morogoro, Songea, Dar es Salaam na Zanzibar, amesema historia hiyo ni fursa inayopaswa kutumiwa kukuza utalii na uchumi wa nchi bila kuingiza mjadala wa udini.
Aidha ameitaka wizara inayosimamia sekta ya utalii kuchangamkia fursa zilizopo na kuhakikisha miradi inayopangwa inaleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amesisitiza kuwa mipango ya Rais inahitaji utekelezaji wenye vitendo na rasilimali, si maneno pekee, akionya kuwa kizazi cha sasa hakitaki kusubiri kwa muda mrefu kwani hakuna Taifa la kesho bila kuchukua hatua leo.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @georgekivumbi tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime