KAMATI YA LISHE GEITA MANISPAA YAKUTANA, MKAZO WAWEKWA KWA AFUA ZA LISHE KWA MAMA NA MTOTO

Halmashauri ya Manispaa ya Geita tarehe 29 Januari, 2026 ilifanya kikao cha tathimini ya mkataba wa Lishe katika Ukumbi wa EPZ – Bombambili kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe ndani ya Manispaa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba amewaagiza Wakuu wa Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kuweka kipaumbele katika kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto kama sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.

Akiwasilisha taarifa Afisa Lishe wa Manispaa, Bi. Pendo Makalangwa amesema Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa akina mama wajawazito na kuimarisha uzingatiaji wa chakula mashuleni.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa, Dkt. Sunday Mwakyusa amesema vituo vya afya vinaendelea kutoa huduma za lishe, elimu ya afya na ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto kwa lengo la kupunguza utapiamlo na udumavu.

Kikao hicho kimeonesha dhamira ya Manispaa ya Geita kuimarisha afya ya mama na mtoto kupitia afua endelevu za lishe.

Na Ekadomaster.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii