Rais Donald Trump wa Marekani amesema siku ya Alhamisi kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin amekubali kusimamisha mashambulizi kwa wiki moja kwenye miji ya Kyiv.
Trump amesema wakati wa kikao cha baraza la mawaziri mjini Washington kwamba hatua hiyo inafuatia ombi lake kwa Putin la kusimamisha mashambulizi, kutokana na baridi kali nchini Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amemshukuru Trump na kuandika kwenye ukurasa wa X kwamba ilikuwa ni taarifa muhimu kutoka kwa rais wa Marekani kuhusiana na uwezekano wa kuhakikisha usalama kwa ajili ya Kyiv na miji mingine ya Ukraine wakati huu wa baridi kali.
Hata hivyo bado haijulikani ni lini hasa usitishwaji huo utaanza na Urusi haijathibitisha matamshi hayo ya Trump.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime