Rais wa Marekani Donald Trump amesema anapanga kufanya mazungumzo zaidi na Iran kuhusu uwezekano wa kupata makubaliano ya nyuklia na kusema huenda asitumie nguvu ya kijeshi dhidi ya taifa hilo.
Baada ya vitisho vya mara kadhaa vya kuivamia kijeshi Iran, Trump jana Alhamisi alisema kwamba tayari wanajeshi wake wanaelekea Iran, lakini anatumai kwa usemba hawatalazimika kuwatumia. Trump alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzindizi wa filamu inayomuhusu mkewe Melania.
Amesisitiza kwamba atakuwa na mazungumzo na Iran na tayari anajipanga kwa hilo.
Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito wa diplomasia katika kusuluhisha wasiwasi unaoongezeka kati ya Iran na Marekani, katikati ya vitisho vya uvamizi wa kijeshi vinavyotolewa na pande zote mbili.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii