Balozi wa Tanzania nchini Italia
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa NGO’s
takribani sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania
mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia.
Mkutano huo ulihudhuriwa
pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa NGO walimpongeza
Mhe. Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya
kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika
kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.
Pamoja na
kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na
ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo
yafanyia kazi. Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara
na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa
ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Balozi wa Tanzania nchini Italia
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akipokea akiwa katika kikao na wadau wa NGO's
mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia.
Balozi
wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye
mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa
Tanzania ni nchi salama ya kufanya shughuli zao.