Watanzania Waonywa Dhidi ya Utapeli katika Ununuzi wa Magari Uingereza

Watanzania wanaokusudia kununua magari kutoka nchini uingereza wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka kutapelewa katika manunuzi ya kimataifa.

Hayo yamebainishwa na balozi wa Tanzania nchini uingereza mhe Mberwa Kairuki wakati akitoa taarifa hiyo ikiwa ni njia bora ya kujilinda dhidi ya udanganyifu na hasara zisizo za lazima.

Amesema ubalozi umepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi waliotuma fedha nchini uingereza kwaajili ya kununua magari, lakini hawajapokea kwa zaidi ya miezi sita hali iliyosababisha hasara na usumbufu mkubwa

Aidha balozi kairuki amewataka waagizaji wa magari kuingia mkataba rasmi wa manunuzi kabla ya kufanya malipo ,kutumia barua ya deni au barua ya udhamini wa malipo badala ya kutuma fedha moja kwa moja hasa malipo makubwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii