Serikali Yatafakari Safari ya Mapambano Dhidi ya Saratani

Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, leo Februari 12 mwaka huu amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Maadhimisho hayo yanafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, yakilenga kutoa fursa kwa taasisi hiyo pamoja na wadau wa afya kutafakari safari ya mapambano dhidi ya saratani nchini.

Kupitia maadhimisho hayo, washiriki wanajadili walikotoka, walipo sasa, na mwelekeo wa baadaye katika kuboresha huduma za kinga, uchunguzi na matibabu ya saratani kwa wananchi.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili mchana  ambapo msomaji wetu wa hii leo ni  @GeorgeKivumbi tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea  mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii