Mji wa Bogodukhiv ni miongoni mwa maeneo ya Ukraine ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakilengwa na mashambulizi ya Urusi hasa katika sehemu za miundombinu ya usafiri na nishati.
Maafisa nchini Ukraine wamesema leo kwamba shambulio la Urusi katika mji wa Bogodukhiv mashariki mwa nchi hiyo limewaua watu wanne, wakiwemo watoto watatu.
Akiutumia mtandao wa kijamii wa Telegram, Mkuu wa jeshi katika mji huo Oleg Synegubov amesema shambulio hilo la anga la Urusi liliilenga nyumba moja na kuwaua watu hao.
Mji wa Bogodukhiv ni miongoni mwa maeneo ya Ukraine ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakilengwa na mashambulizi ya Urusi hasa katika sehemu za miundombinu ya usafiri na nishati.
Hata hivyo ulingana na Ujumbe wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine ni kwamba takriban watu 15,000 wameuawa tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo Februari 2022. Na licha ya juhudi mbalimbali za kuvimaliza vita hivyo vya karibu miaka minne bado nchi hizo mbili zimeendelea kushambuliana.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime