Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kupelekwa kwa wanajeshi hao kutaongeza idadi ya timu ndogo ambayo tayari iko nchini Nigeria ili kusaidia katika kutoa mafunzo,mwongozo wa kiufundi na kufanya mashambulizi.
Ingawa kamandi ya jeshi la Marekani ya Afrika imesema kuwa Marekani itapeleka wanajeshi 200 nchini Nigeria ili kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi ya magharibi mwa Afrika katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi.
Ambapo utawala wa Trump umekuwa ukisisitiza kuwepo kwa matukio ya kulengwa na kuuliwa kwa Wakristo nchini Nigeria ingawa Nigeria yenyewe imekuwa ikikanusha madai hayo na kusema kwamba jamii zote mbili za waikristo na waislamu ni wahanga wa matukio hayo ya kigaidi.
Hata hivyo ni zaidi ya miaka mingi Nigeria imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamekuwa yakiua, yakiteka nyara, kupora na kudai fidia.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime