Spika Justin Muturi Aanika Familia yake Mara ya Kwanza.

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kwa mara ya kwanza, ametambulisha familia yake kwa Wakenya akielekea kutawazwa mgombeaji wa urais wa chama cha Democratic Party katika Ukumbi wa Bomas of Kenya

Muturi, ambaye yuko na ari ya kumrithi Rais Uhuru Kenyatta, alipakia picha akila kiamsha kinywa na familia yake akiitaja kama uti wa mgongo wake katika kivumbi hicho.
Kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, Muturi alichapisha picha zake akiwa pamoja na familia yake kabla ya kuelekea Bomas of Kenya kwa siku yake kuu.
“Tangazo kuu litatolewa baada ya saa chache katika ukumbi wa Bomas of Kenya. Ili kuanza siku hii kuu, nilipata kifungua kinywa na familia yangu. Hakika, familia ndio uti wa mgongo wa kila mtu mkuu na ni nguzo yangu ya usaidizi,” alisema.
Muturi ndiye atapeperusha bendera ya chama cha DP kama mgombeaji wao wa urais baada ya kuidhinishwa kwake leo Jumapili, Februari 20.
Akihutubu wakati wa kuidhinishwa kwake, Muturi alisema Wakenya wanastahili mabadiliko na hayo yatawwezekana tu iwapo viongozi wa uadilifu wanapochukua hatamu za uongozi.
Spika huyo alionyesha matumaini kuwa ana uwezo wa kubadilisha nchi hii akichaguliwa Agosti 9.
Kama ilivyoripotiwa awali, Spika Justin Muturi alisema kuwa serikali yake haitakuwa na huruma kwa viongozi fisadi.
Muturi alipendekeza kuwa viongozi kama hao wanatakiwa kuanikwa kwenye bustani na kisha kuitiwa kikosi cha kufyatua risasi kuwaadhibu.
Alihoji kuwa gharama kubwa za maendeleo zilichangiwa na ufisadi na alipendekeza kwamba sekta muhimu za umma kama vile afya ziendelezwe kikamilifu.
Muturi alishangaa mbona kesi za ufisadi zinachukuwa muda mrefu kortini kabla ya kuamuliwa ilihali ufiadi ndio chanzo cha kuporomika kwa uchumi nchini.

Spika huyo atamenya na kinara wa ODM Raila Odinga na Naibu Rais William Ruto ambao ndio waaniaji wakuu katika kivumbi hicho cha kumrithi Rais Uhuru.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii