Nigeria yanasa tani za ngozi zinazouzwa kama chakula

Mamlaka ya Nigeria inasema kuwa imekamata tani 120 za ngozi za wanyama zilizoagizwa kutoka nje katika jiji la Lagos.

Zilinaswa kwa tuhuma kwamba tayari zilikuwa zimechakatwa na kemikali kwa ajili ya matumizi ya viwanda vya ngozi lakini zilikuwa zikiuzwa kama vyakula, shirika la kitaifa la chakula na dawa, Nafdac, lilisema.

Nchini Nigeria, ngozi ya ng'ombe hupikwa kama kitoweo maarufu kinachojulikana kama "ponmo".

Bado haijabainika zililetwa kutoka nchi gani.

Nafdac ilisema washukiwa saba wamekamatwa.

Iliongeza kuwa uvamizi huo kwenye maghala ulifanywa kufuatia "malalamiko kadhaa" ya wananchi kuhusu usambazaji na uuzaji wa bidhaa hizo ilizotaja kuwa hatari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii