Kane aipeleka Bayern katika hatua ya mtoano

                        Mshambuliaji wa Bayern Munich Harry Kane, ameifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wao                                         wa   2-0 dhidi ya Saint-Gilloise katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo mjini                                               Munich.

Mabao hayo ya Kane yameipelekea Bayern kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora huku wakiwa wamesalia na mechi moja.

Kane nusra afunge mabao matatu ila mkwaju wake wa penalti katika dakika ya 80 uligonga mwamba. Bayern lakini walisalia wachezaji 10 uwanjani kuanzia dakika ya 64 baada ya beki wao wa kati Kim Min Jae kuonyeshwa kadi nyekundu.

Bayern kwa sasa wanaishikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa makundi wa ligi hiyo wakiwa na pointi 18 pointi tatu nyuma ya vinara Arsenal kutoka England ambao hawajapoteza pointi katika jumla ya mechi saba walizocheza.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii