Ikulu ya rais wa Ufaransa ya Élysée
imetangaza kuwa, baada ya kuzungumza na Rais Vladimir Putin wa Russia,
rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron amezungumza kwa njia ya simu pia na
mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kumjulisha kuhusu mazungumzo yao.
Mazungumzo
ya Macron, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya na Putin
yameonekana kutoa fursa ya mwisho ya kuuhitimisha mzozo wa Ukraine kwa
njia za kidiplomasia, huku ikiripotiwa kuwa ukiukaji wa usitishaji
mapigano katika eneo la Donbas mashariki ya Ukraine unaendelea
kuongezeka.
Ofisi ya rais wa Ufaransa imeeleza katika taarifa
kuwa, mazungumzo ya simu kati ya Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo na
rais Vladimir Putin wa Russia yalidumu kwa muda wa saa 1:45.
Putin (kulia) na Macron
Kwa
mujibu wa Ikulu ya Russia, Kremlin, katika mazungumzo aliyofanya kwa
njia ya simu na rais wa Ufaransa hapo jana, Putin ametaka shirika la
kijeshi la NATO na Marekani "zichukulie kwa uzito" madai ya nchi yake
kuhusu usalama wake, ambao ndio kiini cha mzozo wa sasa kati ya Moscow
na nchi za Magharibi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Élysée,
katika mazungumzo hayo ya jana Marais wa Ufaransa Emmanuel Macron na
Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana pia kufanya kila linalowezekana
ili kufikiwa haraka usitishaji mapigano mashariki mwa Ukraine