Morocco imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON 2025 baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1–0 dhidi ya Taifa Stars Tanzania katika mechi iliochezwa katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah, mjini Rabat.
Bao la pekee lilitiwa kimiani kunako dakika ya 64 na Brahim Díaz ambaye ameendelea kuwa mchezaji muhimu kwa wenyeji Morocco kwenye mashindano hayo.
Bao hilo lilikuwa la nne la Díaz katika mashindano hayo na limemfanya awe mchezaji wa kwanza wa Morocco kufunga katika mechi nne mfululizo za AFCON 2025.
Kwa ushindi huo, Morocco sasa itachuana na Cameroon katika hatua ya robo fainali, mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya mataifa hayo mawili kwenye soka la Afrika.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime