Mwanzoni mwa mwaka 2026, Somalia inachukua urais wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kama ilivyo kawaida, baadhi ya viti visivyo vya kudumu katika chombo hiki cha Umoja wa Mataifa hukaliwa na wajumbe wapya kwa mwaka. Miongoni mwao viti hivyo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikirejea zaidi ya miaka thelathini baada ya ushiriki wake wa mwisho katika chombo hiki, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mgogoro wa usalama mashariki.
Nchi tano zitaondoka kwenye Baraza hilo mnamo mwezi Januari 2026: Algeria, Korea Kusini, Guyana, Sierra Leone, na Slovenia. Nafasi zao zimechukuliwa na Bahrain, Latvia, na Colombia, pamoja na wanachama wawili wapya wa Afrika: Liberia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
DRC ambayo ilichaguliwa mnamo mwezi Juni 2025 kama mwanachama asiye wa kudumu kwa muhula wa 2026-2027, ilipata kura 183 kati ya 187 huko New York wakati huo.
Hii ni mara ya tatu DRC kushiriki katika chombo hiki, kufuatia mihula miwili mwanzoni mwa miaka ya 1980 na 1990. "Tutawakilisha sauti ya DRC, lakini pia ile ya Afrika," ametangaza Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Thérèse Wagner.
Kurudi huku kunakuja wakati Kinshasa ikielezea hali ya usalama mashariki kama "vita vya uchokozi vinavyoendeshwa na Rwanda." Mamlaka ya Kongo inalenga kuweka mgogoro huu kwenye ajenda ya Umoja wa Mataifa na kutekeleza Azimio 2773, lililopitishwa mwezi Februari 2025, ambalo linataka kundi lenye silaha la AFC/M23 na vikosi vya Rwanda viondoke kwenye ardhi ya DRC.
Kurudi kwa kidiplomasia
Kiti hiki kisicho cha kudumu ni muhimu kwa diplomasia ya Kongo. Tangu mwanzo wa mgogoro huo, kupata hatua kali kutoka kwa Umoja wa Mataifa "kumeonekana kuwa vigumu kwa Kinshasa," kinakiri chanzo kilicho karibu na ofisi ya rais, hasa kutokana na kusita kwa "kundi la 3A," ambalo linajumuisha nchi tatu za Afrika (Liberia, DRC, Somalia) ambazo si wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.
Kwa kujiunga na kundi hili, Kinshasa sasa inatarajia kubadilisha mwelekeo huo na "kuweka ajenda ya Kongo kwenye meza ya Baraza la Usalama," anaelezea Christian Moleka, mratibu wa chama cha wataalamu wa masuala ya siasa nchini DRC.
Leo, kuna nguvu ya upatanishi na utatuzi wa migogoro nchini Kongo ambayo inaendelea kuvutia umakini wa kimataifa, ingawa vipaumbele vingine vitapewa kipaumbele - pamoja na mvutano wa sasa nchini Venezuela na uwezekano wa mvutano katika Mashariki ya Kati. Kwa hivyo, suala la Kongo linaweza kutoweka mara moja kutokana na hali ya usalama wa kimataifa inayobadilika. Kwa Kongo, ni muhimu kuweka ajenda ya Kongo kwenye ajenda ya Baraza la Usalama ili Azimio 2723, ambalo lilipitishwa kwa kauli moja, liweze kutekelezwa na kupelelekea kurudi kwa amani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime