Kwa mujibu wa Kamandi ya Kusini ya jeshi la Marekani, mashambulizi hayo yalifanyika Jumanne na kulenga msafara wa boti tatu hiuvyo watu wote waliouawa walikuwa ndani ya boti moja.
Jeshi la Marekani limetangaza kuwa watu watano wameuawa katika mashambulizi dhidi ya boti tatu zinazodaiwa kusafirisha dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la bahari.
Kwa mujibu wa Kamandi ya Kusini ya jeshi la Marekani, mashambulizi hayo yalifanyika Jumanne na kulenga msafara wa boti tatu ambapo watu wote waliouawa walikuwa ndani ya boti moja.
Eneo hasa la tukio halijawekwa wazi ingawa mashambulizi ya awali yamewahi kufanyika Karibiani na Pasifiki ya Mashariki. Jeshi linasema boti hizo ziliendeshwa na “makundi ya kigaidi,” bila kuyataja majina.
Tangu Septemba, Marekani imefanya zaidi ya mashambulizi 30 ya aina hii, hatua inayokosolewa na wataalamu wa sheria za kimataifa kama mauaji ya nje ya sheria.
Haya yanajiri wakati Rais wa Marekani Donald Trump akiendelea kuishinikiza Venezuela akimtuhumu Rais Nicolas Maduro kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya—madai ambayo Maduro anayakana.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime