Mourinho awapa maua yao wachezaji kutoka Afrika

Miongoni mwa Kocha bora duniani Jose Mourihno (The Special one) katika moja ya mazungumzo yake na Rio Ferdinand amefunguka kuhusu wachezaji wa Afrika.

"Siwezi kwenda Afrika, nina mashabiki wengi huko… na kila mahali kwa ujumla, Nimewahi kuwafundisha wachezaji kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kama.

Drogba na Salomon Kalou kutoka Côte d'Ivoire, Geremi na Samuel Eto'o kutoka Cameroon, Obi Mikel kutoka Nigeria, Essien na Sulley Muntari kutoka Ghana”

“Kila ninapokwenda Afrika, siwezi kutembea kutembea. Watu wananionyesha upendo makubwa sana, wachezaji wa Afrika ni waaminifu sana” – Mpurinho

"Kusema kweli, nawapenda Waafrika na hasa wachezaji wao. Mchezaji huyo wa Kiafrika ni mwaminifu sana. Baadhi ya wachezaji huniita 'baba', kama Michael Essien, ingawa wana umri karibu nami!.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii