Michuano ya AFCON 2025 imeendelea kuwasha moto nchini Morocco na sasa picha ya nani anaweza kusonga mbele hatua ya 16 bora inaanza kuonekana kwa baadhi ya vigogo wameonyesha ubabe huku timu nyingine zikibaki kupigania nafasi ya mwisho ya kuokoa heshima.
Na huu hapa ni muhtasari wa msimamo wa kila kundi:
Group A
Morocco imeanza vizuri na kuendelea kuongoza kundi, ikifuatwa kwa karibu na Mali na Zambia ambao bado wana nafasi ya kusonga mbele.
Morocco — 4 pts
Mali — 2 pts
Zambia — 2 pts
Comoros — 1 pt
Group B
Misri (Egypt) imeonesha ubora wake — pointi zote 6, ikionekana kuwa tayari kwa hatua ya mtoano.
Egypt — 6 pts
South Africa — 3 pts
Angola — 1 pt
Zimbabwe — 1 pt
Group C
Nigeria ipo kileleni baada ya kushinda michezo yake, huku Tanzania na Uganda zikibaki kupambana.
Nigeria — 6 pts
Tunisia — 3 pts
Tanzania — 1 pt
Uganda — 1 pt
Group D
Hili kundi lina ushindani mkubwa — Senegal na DR Congo ziko juu kwa pointi sawa.
Senegal — 4 pts
DR Congo — 4 pts
Benin — 3 pts
Botswana — 0 pts
Group E
Algeria tayari imejihakikishia 16 bora baada ya matokeo bora.
Algeria — 6 pts
Burkina Faso — 3 pts
Sudan — 3 pts
Equatorial Guinea — 0 pts
Group F
Kundi hili limechanganya — timu tatu zina pointi sawa.
Ivory Coast — 3 pts
Cameroon — 3 pts
Mozambique — 3 pts
Gabon — 0 pts
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime