IKULU YATANGAZA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI

Ikulu ya Tanzania jana imetangaza mabadiliko katika Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Rais Samia amemteua Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya George Simbachawene ambaye ametenguliwa  hivyo kabla ya uteuzi huo Katambi alikuwa akihudumu kama Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Katika mabadiliko hayo Rais Samia pia amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Ikulu (Kazi Maalum). Profesa Kabudi kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Nafasi ya Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Profesa Kabudi sasa imechukuliwa na Paul Makonda, ambaye awali alikuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo.

Mabadiliko hayo ni sehemu ya jitihada za Rais Samia kuimarisha utendaji wa Serikali na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii