Maduro ajitetea mahakamani baada ya kukamatwa na Marekani

Kiongozi wa Venezuela Nicolás Maduro amejitangaza kuwa "rais halali wa Venezuela" wakati akipinga kukamatwa kwake nchini Marekani na amekanusha mashtaka mazito ya usafirishaji wa dawa za kulevya.

Nicolás Maduro amejitangaza kuwa "rais wa Venezuela" wakati alipokuwa akipinga kukamatwa kwake na amekanusha mashtaka ya usafirishaji wa dawa za kulevya, mashtaka ambayo utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump ulitumia kuhalalisha kuondolewa kwake madarakani.

Akiwa mahakamani mjini Manhattan, Maduro alisema kwa lugha ya Kihispania - kupitia mkalimani kwamba "alikamatwa", kabla ya jaji kumkatiza.

Alipoulizwa msimamo wake kuhusu mashtaka yanayomkabili, Maduro alisisitiza kuwa hana hatia, ni mtu mwadilifu, na kwamba bado yeye ndiye rais halali wa nchi yake.

Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufikishwa mahakamani Manhattan tangu yeye na mkewe, Cilia Flores, walipokamatwa nyumbani kwao Caracas Jumamosi katika operesheni ya kijeshi ya kushtukiza. Flores pia amekana mashtaka.

Kukamatwa kwa Maduro kumetajwa na wachambuzi kama tukio lisilo la kawaida katika historia ya mahusiano ya kimataifa, kwani ni nadra kwa kiongozi wa taifa kufikishwa mahakamani nchini Marekani kwa mashtaka ya uhalifu wa kimataifa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii