JKT Queens yaifuata Ceasiaa Iringa

KIKOSI cha mabingwa watetezi JKT Queens kimeondoka jijini Dar es Salaam jana kuelekea Iringa ili kuwafuata wenyeji Ceasiaa Queens kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania itakayochezwa Desemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mkoani humo.

Msemaji wa timu hiyo Masau Bwire alizungumza na vyombo vya habari kuwa  wachezaji wote wana morali ya juu kuelekea katika mchezo huo na wanakwenda huko kwa lengo moja la kusaka pointi tatu muhimu. 

Bwire alisema watacheza kila mechi kama fainali kwa sababu wanataka kutetea ubingwa na kurejea tena katika michuano ya kimataifa mwakani. 

Aliongeza kwa kusema kuwa wanafahamu itakuwa mechi ngumu na yenye upinzani, lakini hawana hofu yoyote kwa sababu wamejipanga kwenda kupambana.

Wakati huohuo Simba Queens pia imeondoka jijini Dar es Salaam jana kuelekea Manyara kuwafuata wenyeji wao Fountain Gate Princess.

Meneja wa Simba Queens, Selemani Makanya, alisema jana wanakwenda mkoani humo na kikosi kamili kwa sababu wanafuata ushindi. 

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii